Jan 2, 2010

abdulmutallab

huyu abdulmutallab toka nigeria sijui mwendawazimu au nini? washenzi washenzi kama huyu ndiyo wanaofanya kusafiri kwa ndege kuwe kugumu. kwa sababu lazima tu wamarekani sasa wataongeza nuksi kwenye safari. ubaya wake ni kuwa watakaopata tabu zaidi si waarabu peke yao bali pia wanaigeria na hasa wenye majina ya kiarabu.

tatizo kubwa zaidi ni kwamba na siye wasafiri wengine wengine tusiokuwa wanaigeria, waarabu au waislamu na wala tusio na majina ya kiarabu tutaonewa bila sababu na hakuna mmoja wetu mwenye sauti ya kulalamika akasikilizwa. kwani ukisema fyoko basi na wewe utakiona kilichomtoa kanga manyoya. uwe umeonewa au la. juwa wazima hawa wamarekani wakidhani wanalinda maslahi yao hawamjali mtu yeyote yule asiyekuwa wao. hata ulie machozi ya damu.

haya basi tuone itakuwaje.