May 16, 2011
usanii wa wasirikali
du!! tutakoma ubishi. kwa sababu kikwete na wakali wake wametuletea mpya zaidi na wanatukweta bila hata ya huruma. hala hala yasije tokea kama yaliyomkuta acheampong ghana. kwa vijana wetu wasiojua historia, nazungumzia baada ya watu wake kumtoa kwenye kiti kijeshi wakamtupia lawama zote yeye wakidai kuwa aliruhusu uozo usambae na kuota mizizi na kuacha rushwa na wizi wa kimasomaso kuwa kitu cha kawaida.
chonde ndugu zangu. . .
May 10, 2011
zamu yetu kula
Jan 2, 2010
abdulmutallab
tatizo kubwa zaidi ni kwamba na siye wasafiri wengine wengine tusiokuwa wanaigeria, waarabu au waislamu na wala tusio na majina ya kiarabu tutaonewa bila sababu na hakuna mmoja wetu mwenye sauti ya kulalamika akasikilizwa. kwani ukisema fyoko basi na wewe utakiona kilichomtoa kanga manyoya. uwe umeonewa au la. juwa wazima hawa wamarekani wakidhani wanalinda maslahi yao hawamjali mtu yeyote yule asiyekuwa wao. hata ulie machozi ya damu.
haya basi tuone itakuwaje.
May 21, 2007
wanyang'anyi
inasemekana hivi sasa ardhi ni rasmali kubwa
ni kumpa mjumbe wa nyumba kumi kiasi kadhaa au kumnywesha kangara, chibuku au bia mbili tatu atie dole gumba. ukishtuka unaambiwa kwamba sirikali imeigawa sehemu yako kwa sababu umeshindwa kuihudumia. na huna pa kwenda. kwani kila utakapokwenda ni mizunguko mizinguo tu ndiyo haiishi. pengine unayeongea naye ni shemeji yake huyo bosi aliyemuhonga mjumbe.
“njoo kesho, bosi hayupo. njoo kesho … njoo kesho.” utachoka mwenyewe. kufuatana na niliyosikia na kushuhudia, nchi ya kikwete na hawa wezi wezi wengine hivi sasa haina tofauti kubwa na za zamani. watu wasio na chao wanakwetwa
swali, je, watu waliokuwa wakiishi pale wameishia wapi? na walipata fidia ya kutosha au kuridhisha, kufuatana na walichopoteza? au ndiyo walifanyiwa kiini macho tu? na
ni kweli kuwa hali hii iko afrika nzima. kwa mafno msumbiji mawazir walikuwa akinunua mabsha makubwa na ardhi na kuiwekeza hadi hapo bei itakapopanda halafu wanauza kwa faida ya ajabu. lakini tunazungumzia rasmi bongo. nchi ambayo inajigamba kwa kuwa salama na isiyo na shida za ubaguzi na matatizo ya uhasama wa kidini. ukabila. na matatizo mengine
hii ni amri ya sirikali aua watu fulani tu wajanja wajanja waliopewa majukumu ya kuangalia mashamba na ugawaji/ uuzaji wa mashamba na viwanja? je, huu si wizi wa kimasomaso? na yote hii ni kutokana na unyonge wa wale wanaochaguliwa na kuporwa haki zao. wenye pesa sehemu zao haziguswi kamwe. sasa haki na usawa viko wapi?
navyoona mimi sirikali ingewaambia watu kuwa maeneo
mwalimu alishindwa na ujamaa wake. sababu kubwa ni kuwa watendaji wa kanuni zake walikuwa wakitenda kinyume au shingo upande. kwani walikuwa wakiona uhondo unawapita tu hivi hivi walipofananisha na wenzao wa
kweli kuna majumba ya maghorofa marefu ya chuma na vioo na watu wengi wana tv (za hali duni), magari ya kupendeza na kuvutia (kupendeza hakumaanishi ubora). kwa wengine, wengi wasioelewa na wenye akili finyu, haya ni maendeleao. lakini maendeleo hasa ni watu na siyo vitu.
swali, ukabaji huu utakaposhindwa, au wananchi wakichoka kuonewa na kunyanyaswa, sulushisho litakuwa nini?
sidhani tena, na ni wazi,
walio baki alamsiki.
Apr 29, 2007
viongozi jina
juzi niliona picha ya watoto wa kibongo wakiwa darasani (http://harakati.blogspot.com/). jambo la kusikitisha ni kuwa, inavyosemekana, mbunge wa sehemu hiyo ni mmoja kati ya waliootesha mizizi bungeni na mtu mwenye nafasi serikalini. lakini hakuna chochote alichokifanya hadi sasa. watu wake, ambao ndiyo waliomchagua na kuendelea kumchagua, hawaelewi lolote (na
niwazi kuwa watu fulani wananufaika zaidi ya wengine kwa jinsi hali ilivyo. na inavyoendelea kubaki hivyo ndiyo wanavyozidi kuvimbiwa. wakati wachovu wanazidi kufa kwa njaa na maradhi. dhahiri viongozi hawa hawaoni aibu wala kujisikia vibaya kwa kuwakandamiza ndugu zao. hali hii itaendelea mpaka lini?
Jan 15, 2007
tumeingiliwa
hali halisi
kweli kila mtu ana haki na uhuru wa kuabudu dini yeyote au anavyotaka. lakini, hii ni kwa maneno tu. hali halisi si kweli kwamba kila mtu anafuata dini anayotaka au kuipenda. au kuwa na haki ya kutofuata kabisa dini yoyote ile kati ya hizi nyingi za kigeni na zilizopewa umashuhuri.
ukweli uliowazi ni kwamba kuna watu wamejipa uwezo wa kimungu mungu. wengi wanasiasa au washabiki tu wadini wanaofuata na kuipigia debe dini fulani. wanajifanya na kujiona
swali. hivi hawa ndugu zetu wanoleta unoko kwenye ukristu na kujifanya wajuzi wa dini hii, wangapi kati yao wanaojua kuwa jina la yesu ni jina tu la kawaida (ambalo hutamkwa hee-sus) katika nchi zinazongumza lugha ya kispanish? na wangapi wanaojua kuwa katika enzi za utumwa, au tuseme wazungu kuleta utumwa afrika, moja ya meli mashuhuri sana katika biashara hii ilijulikana kwa jina la jesus christos - jina la yesu kilatini? kasome.
dini hizi zote ni za kigeni, kwa jinsi tuzijuavyo na zilivyoletwa afrika. (kuna wataalamu wa historia wanaodai kuwa dini zote hizi zina asili ya kiafrika). waafrika walikuwa na imani zao na taratibu za kutimiza na kufuata kanuni za imani hizo. kulikuwa na sehemu ya kufanyia sala, maombolezi au tambiko. iwe kusali chini ya mbuyu. mkuyu. mugumo. au kando ya mtoni. waislamu wana taratibu zao na wakristo nao. sasa inakuwaje za wengine (ambazo ni ngeni) zionekane bora zaidi, na kumlazimisha kila mtu kuzifuata hizo, na kuzitelekeza zao za kijadi? kwa misingi gani?
hawa wanaolazimisha watu kufuata uislamu kwa mijeledi, walipewa na nani uwezo huu? kweli allah anakubaliana na itikadi hizo? na mtu anayefuata dini kwa kuogopa mijeledi, je, huyu ana imani au anafuata mkumbo kwa kuogopa njukuti? yaani kuchapwa mikwaju na mtumwa aliyekula akashiba msikitini?
na hawa wanojifanya walokole, ili wawachune na kuwala walala hoi senti zao, je? wakati wanapata pesa za omba omba wanajidai kuhubiri na kuwapotosha wafuasi wao. ni lazima, ili wapewe chochote na wafadhili toka ulaya na marekani, waonyeshe kuwa kweli wanahubiri na kuwaingiza watu katika ufuasi wa yesu, hivyo ni muhimu
hii haina tofauti na wanasiasa wanaoendeleza na kukuza kasumba ya omba omba toka ulaya. wakipata marupurupu asilimia 90% wanaiacha ulaya walikochimbia hazina zao za wizi na kuleta sehemu ndogo
katika filamu moja ya marehemu mzee usmane sembene (mungu na mizimu wamuweke pema) - iitwayo guelwaar, ambalo ni jina la mtu aliyekuwa mpigania haki za watu wake - guelwaar anasema, "sote tunajua kuwa ukiweka mikono mbele na kukunjua kidole kimoja kwenye ngumi, unaonyesha njia au kuelekeza. lakini ukiweka vidole vyote wazi, basi unaomba. na mtu aliyezoea kuomba na kupewa kila siku anajua maneno mawili tu, jaali jef - au "asante sana" kwa kiwolof cha sunugal.
ni wazi kuwa pazia tuliyowekewa usoni ni nzito kiasi kwamba si rahisi kuona janja ya wanaojifanya wadini na wanasiasa wa uongo na kweli. sababu kubwa ya kuwaingiza kwenye siasa na dini siyo kuleta mabadiliko, bali kutunisha vitambi na mifuko
tufumbue macho waajameni. iwe dini iwe siasa. tunapozugwa tushituke. au tuwe macho zaidi ili tusizugwe kirahisirahisi. dini ni imani. fuata dini unayotaka. fuata chama unachotaka au muunge mkono mwanasiasa umpendae. ila usinilazimishe mimi. ntafanya na kufuata kile moyo wangu unachonituma, ili muradi sivunji sheria na raha yangu haimbugudhi mtu mwingine. vinginevyo niache
ndumila kuwili
hawa watu wanojifanya watakatifu, au kupewa utakatifu na wapambe wao, au watu wengine wengine tu, pengine majumbani kwao ndiyo kuna uovu usiosemekana. je, nani atakaye wahukumu wao? mara ngapi tunasikia kuhusu shehe nanihii kamdunga selemani au kijana fulani mtiifu na mwenye imani na ari kubwa ya kutaka kujua mafunzo ya kitabu kitakatifu? au ya kuwa shehe nonihino kawaweka kinyumba watoto wa kiume au wakike, ati wanafunzi wake. na, je, vipi kuhusu padri, father stephen lugomba, au buruda stanslaus rogue? wakatoliki wanatakiwa wasioe, lakini yeye ana kina dada kadhaa (wapenzi wa biblia wanaoimba kwaya) wanaompa burudani baada ya sala ya jioni?
ndumila kuwili hawa atawahukumu nani? maalim vikapu kashawapa amri vijana wa mtaa waende kona ya mtachoka na ufukweni kuwachabanga magumi watu wa kijiwe kwa sababu wana pepa sayo. kwa nini kuvuta bangi ni kuvunja sheria lakini kunywa pombe si kuvunja sheria? wa kijiweni wanapigwa vita ati saa zote wanalikoleza badala ya kijiendeleza kimaisha - wakati hakuna kazi hata kwa waliosoma, kwa sababu ya undugunization. mbona shehe kurandaranda (na kanzu yake ambayo zamani ilikuwa nyeupe) haulizwi? muhishiwa shehe mlawiti, au padri japhet kambong'oza, kapewa na nani haki ya kuwahukumu wavuta bangi, wakati yeye mwenyewe anavunja sheria zaidi na mdhambi yake ni makubwa kuliko? na kila jumangapi lazima apate chupa kadhaa.
wao wenyewe wanakwenda kinyume cha vitabu vyao vitakatifu. kama si undumila kuwili basi ni nini? na vipi bado wana uwezo wa kuwahukumu wengine kwa makosa ambayo wao wenyewe ndiyo waovu zaidi. shehe na padiri walevi zaidi ya watu wanaowatuhumu kwa niaba ya dini zao. ukiangalia picha hii ina kasoro gani?
wapi kwenye vitabu hivi vitukufu inasema kuvuta bangi si halali? au kunywa pombe ni halali? (wala usifikirie vipi, mimi sinywi wala sivuti). na wapi inasema kasisi au shehe anaruhusiwa kukata kiu mara moja moja, kuwainamisha watoto wasiojua kitu na kuwatubisha kinamna?
tumeingiliwa na mdudu wa akili anayetufanya tuchukiane na kuuana bila sababu kutokana na dini za watu. kina mama wanalazimishwa kuvaa maguoguo, ati kwa sababu shehe nanihii karudi toka pakistani na wanawake wakipakistani,
sidhani
swali, shehe anayekwenda kuhiji kwa nauli aliyoipata kwa biashara ya magendo au kumzika kalimanzila hela zake za dagaa, au njia haramu anazozijua yeye (na kisheria), anapata thawabu?
kabla hujamtupia jiwe mtuhumiwa kwa uasherati, jiangalie kwa makini wewe mwenyewe. ni msafi na umetakata kiasi hicho? na unatupa jiwe
umeshaona dhahabu zinazoipamba
dini yangu. naamini mungu. au miungu. awe olodumare. buda. nzambe. nkulunkulu. nyame. shango. nguluvi. jah - rastafari. au nanabizhou. usinong'one wala kunizungumzia, ati mkafiri. afrika hakuna makafiri. makafiri wako kwenye akili za wanaotunga haya maneno tu. mimi ngangali. ungangali wangu unatokana na kulindwa na obatala. ogun. na mizimu yangu (iliyoko nyumba nitu na kwingineko)na kwa uwezo wa muumba. au waumba. kwa sababu naamini mungu. au miungu. wangu anajua na kuongea lugha nyingi. si kiarabu tu peke yake. au kirumi na kizungu kingine. lugha zote ni zake. au zao. vinginevyo sala zangu. mizimu yetu. zingejibiwa vipi? mungu (awe mmoja au wengi) ndiyo dini pekee nayoijua.
hizi nyingine biashara tu.
Dec 24, 2006
utu wa mtu
kila nikiangalia pande mbali mbali za afrika, na hasa mijini, naona ubinadamu unazidi kupungua tu. watu hawawajali wenzao
wakati nchi za kiafrika zinazidi kuwa fukara, kwa kukamuliwa na wababe wa kimarekani na wazungu wengine, viongozi wa kiafrika (vikaragosi wao) wanatuna wakati wananchi wao wanazidi kukondeana kwa umaskini. wakati huo huo nchi hizi hizi, zijulikanazo
kwa mfano kulikuwa na habari kuwa raisi wa zamani wa
wengine wanajidai kuvutia utandawizi kwa kukaribisha wawekezaji. tushawashitukia, janja
hala hala kesho kuna moto wajameni.