May 21, 2007

wanyang'anyi

inasemekana hivi sasa ardhi ni rasmali kubwa sana bongo. ukweli ni kwamba siku zote ardhi ni raslimali, isipokuwa sasa ni mara dufu ya wakati mwingine wowote ule. kwa hiyo wasirikali wamekuwa wanyang’anyi zaidi. kwa kawaida wanavamia mashamba ya wachovu na kudai kuwa wanaweka mapori. wenye pesa wakikodolea macho sehemu yako basi ishaondoka unapopatikana upenyo.

ni kumpa mjumbe wa nyumba kumi kiasi kadhaa au kumnywesha kangara, chibuku au bia mbili tatu atie dole gumba. ukishtuka unaambiwa kwamba sirikali imeigawa sehemu yako kwa sababu umeshindwa kuihudumia. na huna pa kwenda. kwani kila utakapokwenda ni mizunguko mizinguo tu ndiyo haiishi. pengine unayeongea naye ni shemeji yake huyo bosi aliyemuhonga mjumbe.

“njoo kesho, bosi hayupo. njoo kesho … njoo kesho.” utachoka mwenyewe. kufuatana na niliyosikia na kushuhudia, nchi ya kikwete na hawa wezi wezi wengine hivi sasa haina tofauti kubwa na za zamani. watu wasio na chao wanakwetwa sana. inasemakana mkwete ana sehemu kubwa sana tu kisarawe au sehemu fulani, ambayo aliipata kimizengwe.

swali, je, watu waliokuwa wakiishi pale wameishia wapi? na walipata fidia ya kutosha au kuridhisha, kufuatana na walichopoteza? au ndiyo walifanyiwa kiini macho tu? na kama sivyo walilalamika wapi? walisikilizwa?

ni kweli kuwa hali hii iko afrika nzima. kwa mafno msumbiji mawazir walikuwa akinunua mabsha makubwa na ardhi na kuiwekeza hadi hapo bei itakapopanda halafu wanauza kwa faida ya ajabu. lakini tunazungumzia rasmi bongo. nchi ambayo inajigamba kwa kuwa salama na isiyo na shida za ubaguzi na matatizo ya uhasama wa kidini. ukabila. na matatizo mengine kama hayo. lakini, je, nani anayezungumzia unyang’anyi huu wa ardhi za walala hoi? kama kweli maeneo fulani hivi sasa (kutokana na maendeleo, makuzi na matanuzi ya jiji) si maeneo ya mashamba tena, kwa nini sirikali isiwaambie watu wauze sehemu zinazowashinda kujenga? badala yake wananyang’anywa maeneo yao na sirikali, ambayo inayauza na kutia ndani pesa.

hii ni amri ya sirikali aua watu fulani tu wajanja wajanja waliopewa majukumu ya kuangalia mashamba na ugawaji/ uuzaji wa mashamba na viwanja? je, huu si wizi wa kimasomaso? na yote hii ni kutokana na unyonge wa wale wanaochaguliwa na kuporwa haki zao. wenye pesa sehemu zao haziguswi kamwe. sasa haki na usawa viko wapi?

navyoona mimi sirikali ingewaambia watu kuwa maeneo yao hivi siyo mashamba tena na ya kuwa wanatakiwa wejenge nyumba za kuishi, iwapo watashindwa basi sirikali itazigawa sehemu hizo ili ziuzwe kama viwanja. halafu itakata asilimia ndogo ili kujilipa fidia kwa huduma ya kugawa mashamba kitaalamu kuwa viwanja. wala siyo kuuza tu mashamba ya watu na kubaki na pesa. huu ni unyang’anyi, dhuluma na kuwanyima haki wenye mashamba. kitu ambacho kimekua cha kawaida sana sasa bongo.

mwalimu alishindwa na ujamaa wake. sababu kubwa ni kuwa watendaji wa kanuni zake walikuwa wakitenda kinyume au shingo upande. kwani walikuwa wakiona uhondo unawapita tu hivi hivi walipofananisha na wenzao wa kenya na nchi nyingine. matokeo yake ukabaji usiotumia silaha na unyonyaji, ambao wengi waliupenda tokea enzi, ndiyo ukapewa nafasi na sifa zote kwa madai kuwa ujamaa ulishindwa na kurudisha nchi nyuma (kama alivyoda njonjo).

kweli kuna majumba ya maghorofa marefu ya chuma na vioo na watu wengi wana tv (za hali duni), magari ya kupendeza na kuvutia (kupendeza hakumaanishi ubora). kwa wengine, wengi wasioelewa na wenye akili finyu, haya ni maendeleao. lakini maendeleo hasa ni watu na siyo vitu.

swali, ukabaji huu utakaposhindwa, au wananchi wakichoka kuonewa na kunyanyaswa, sulushisho litakuwa nini?

sidhani tena, na ni wazi, kama watu watataka kurudia ujamaa baada ya kuonja buyu la asali ya unyonyaji na ukandamizi wa wenzao wasio kitu. halahala walio lala wasiamke. vinginevyo, hatimaye, vumbi na manyoya yakishatulia, mwenye nguvu ndiyo atakayebaki kasimama.

walio baki alamsiki.

No comments: